Alhamisi 18 Juni 2026 - 20:54
Abu Alaa Al-Wala’i: Sauti ya “فُزنا وربّ الكعبة” Imesikika Katika Uwanja Mzima wa Muqawama

Hawza/ Katibu Mkuu wa Kataib Sayyid al-Shuhadaa (as) nchini Iraq, akisisitiza kwamba; leo sauti ya “فُزنا وربّ الكعبة” imetanda katika uwanja mzima wa muqawama, amesema: Kupitia kutimia kwa “Ahadi ya Kweli” (Wa‘d Sadiq) na ushindi wa kihistoria wa Iran, imethibitika tena kwamba; wana wa muqawama kamwe hawatakubali maridhiano ya kujisalimisha, na wataendelea kushikamana kwa uthabiti na ahadi yao kwa mashahidi Khamenei na Nasrullah.

Kwa mujibu wa Kitengo cha Kimataifa cha Shirika la Habari la Hawza, Abu Alaa Al-Wala’i, katika ujumbe wake wa hamasa uliochapishwa kwenye mtandao wa X katika siku za kuelekea kutangazwa kwa makubaliano kati ya Tehran na Washington, alizungumzia nafasi ya juu ya ustahimilivu wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran mbele ya maadui wake na kusema: “Leo tupo katikati ya tukio kubwa la kihistoria. Muqawama wa Kiislamu wa Iraq, kupitia juhudi na mapambano yake katika njia ngumu ya Dhāt ash-Shawkah, umeandika ukurasa wenye kung'ara katika ushindi huu na umeweka mchango wake kwa herufi za nuru katika historia ya heshima ya Umma wa Kiislamu.”

Alieleza kwamba; irada ya chuma ya mujahaidina ndiyo iliyokuwa sababu kuu ya kuvuka vikwazo vigumu zaidi, na akaongeza: “Subira na ustahimilivu wa wapiganaji hatimaye vimezaa matunda, na kwa kufikiwa kwa malengo makubwa, Ahadi ya Kweli imetimia.”

Katibu Mkuu wa Kataib Sayyid al-Shuhadaa (as), akiendelea na hotuba yake huku akifanya upya ahadi kwa makamanda mashahidi wa muqawama, alisisitiza: “Tukimuelekea shahidi mtukufu Imam Khamenei, na lulu ya Lebanon shahidi Sayyid Hassan Nasrallah, pamoja na mashahidi wote wa njia hii yenye baraka, tunatangaza kwamba; bado tumesimama imara juu ya njia ileile; na katika msamiati wetu hakuna hata chembe ya kurudi nyuma wala kufanya maridhiano.”

Mwishoni, Al-Wala’i alihitimisha ujumbe wake kwa kauli ileile ya ushindi:

«فُزنا وربّ الكعبة»

“Naapa kwa Mola wa Al-Kaaba kwamba tumefaulu na tumepata ushindi.”

Abu Alaa Al-Wala’i: Sauti ya “فُزنا وربّ الكعبة” Imesikika Katika Uwanja Mzima wa Muqawama

Lebo

Maoni yako

You are replying to: .
captcha